Sunday, June 22, 2014

DR. MARY MWANJELWA; MWANAMKE SHUPAVU WA SIASA ZA VITENDO

Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa -MB, akitoa mada juu ya kumwezesha mwanamke na uongozi katika maamuzi kwenye Bunge la ACP-EU Women Forum Brussels-Belgium Jumamosi tarehe 15/6/2013



UNAPOPATA kujua historia za wanasiasa wanawake nchini Tanzania wanaofanya vizuri katika majimbo ama mikoa yao, ni dhahili huwezi kukosa jina la Dr. Mary Mwanjelwa.

Mwanamke huyo ni Mbunge wa Viti maalum kutokea mkoani Mbeya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Sifa yake ya kwanza ni ucheshi ambao yeye anasema kuwa ucheshi wake unatokana na wokovu alionao(kumcha Mungu).

Kabla ya kujikita katika masuala ya siasa alikuwa Mkurugenzi wa shirika la PSI Tanzania ambako historia haimuhukumu hata baada ya kutoka huko kwa kile kinachojieleza kuwa alitoka na utumishi uliotukuka.

Katika mahojiano na Mwandishi wa makala haya, Dr. Mary Mwanjelwa anasema kuwa alipata ubunge kupitia viti maalum mwaka 2010.

Anasema kwa sasa katika mkoa wa Mbeya, kuna wabunge wa viti maalum wawili ambao ni yeye na Hilda Ngoye.

‘’Najivunia nafasi niliyonayo maana imenipa na nafsi ya kuwa Mbunge wa Bunge la Ulaya nikiwakilisha Tanzania’’ anasema Dr. Mwanjelwa.

Alipoulizwa kuwa tangu achaguliwe kuwa Mbunge wa mkoa huo amefanya nini cha kujivunia mpaka sasa, alisema ameweza kuwainua makundi mbalimbali hasa wanawake wa wilaya zote za mkoa wa Mbeya.

Anasema anapenda sana kushiriki katika shughuli za kimaendeleo za jumuiya na hata familia moja moja.

‘’Kuanzia mwaka 2010, kwa kukumbuka baadhi ya niliyoyafanya ni pamoja na kujumuika na kuwasaidia yatima,  kusaidia vikundi vya akina mama na kufadhili semina za madiwani wa vyama vyote juu ya utendaji bora’’ anasema Dr. Mwanjelwa.

Elimu.
Anataja maeneo ambayo amewahi kujumuika na jamii kuhusu elimu kuwa ni kushona sare za shule nguo na viatu kwa watoto yatima 100 kata za Kambasegele na Kiwira wilayani Rungwe.


Anasomesha watoto yatima 2 wa kike kila wilaya za mkoa wa Mbeya ambazo ni Mbeya mjini, Kyela, Rungwe, Mbeya Vijijini, Mbarali, Chunya, Ileje na Mbozi.

Si hayo tu bali nimesaidia ujenzi wa sekondari kata ya Itagano-Jiji la Mbeya, mifuko ya saruji tani Moja, ujenzi wa sekondari ya kata ya Ruanda saruji tani Moja na niligawa vitabu katika sekondari 9 zote za mkoa wa Mbeya, kila wilaya shule Moja na Kugawa vitanda 19 katika hosteli ya wasichana Sekondari ya Isansa ’’ anasema Mbunge huyo.

Ujasiliamali
 
Anasema amefanikiwa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kwa kina mama kila wilaya -zote za mkoa wa Mbeya na  kufadhili Mashine za kutotolea vifaranga na kutoa pesa za mitaji wilaya zote za mkoa wa Mbeya.

‘’Nilitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa kina mama juu ya incubators hizo nilizowafadhili ili waweze kuendelea kujitegemea katika kukuza uchumi wao badala ya kuwa wategemezi kila wakati na niliendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wana Mbeya kwa kuzingatia jinsia’’ anasema Mbunge huyo.

Aliwezesha kaya 300 mbuzi wawili wawili  kaya -kata ya Kambasegela na Kiwira wilayani Rungwe.

Afya
Anaeleza kuwa ni mambo mengi ya jamii aliyoshiriki na mengine ameyasahau lakini anakumbuka pia aligawa magodoro 250 katika hospital za serikali katika wadi za wazazi wilaya ya Ileje, Mbozi, Chimala(Mbarali), Ruanda na hospitali ya Rufaa ya Mbeya kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya.

Aidha anasema amegawa vitanda 19 katika hosteli ya wasichana Sekondari ya Isansa iliyopo wilayani Mbozi, kutoa gari ya sinema katika Jiji la Mbeya juu ya uelimishaji Umma katika Tiba kwa Kadi kupitia mfuko wa Bima ya afya ya Taifa(NHIF).

Kushiriki kampeni ya kufanya usafi katika Jiji la Mbeya.

‘’Nilitoa vyakula katika vituo cha watoto yatima cha Iwambi na kugawa nguo na mablanketi katika kituo cha watoto yatima cha Uyole vyote vya Jijini Mbeya’’ anasema Dr. Mwanjelwa.

Sanjali na vitu hivyo, anasema kuwa alitoa pia viti vya walemavu wa viungo katika Jiji la Mbeya mbele ya Askofu kiongozi wa kanisa la Moravian Tanzania Alinikisa Cheyo siku alipkuwa akimshukuru Mungu kwa kumponya na mauti katika ajali mbaya aliyoipata mwaka jana 2012.

Uongozi.

Katika masuala ya uongozi, anasema aliendesha na atazidi kufanya hivyo kwa kufadhili mafunzo/semina za mara kwa mara kwa Madiwani wote wa Mkoa wa Mbeya, juu ya Uongozi na uwajibikaji.

‘’Mbali na mafunzo ya madiwani hao, nimewahi kuendesha mafunzo/semina kwa watendaji wote wa ngazi ya kata juu ya Uongozi na uwajibikaji na nitazidi kufanya hivyo’’ anasema.

Anajipambanua kuwa pia amewahi kuendesha mafunzo/semina kwa wenyeviti na makatibu wa umoja wa wanawake wa chama chake UWT katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya jinsi ya Uongozi na Uwajibikaji.

Mbali na kazi za kijamii, anasema mara kadhaa huwa anashiriki kazi za kusaidia vikundi, waimbaji na hata makanisa ambapo hivi karibuni alitoa vyombo vya Muziki Kanisa la Ruanda Moravian kwaya Kuu Jiji la Mbeya.

Mbali na makanisa anaeleza kuwa anashiriki pia kusaidia michango mbali mbali ya kijamii kama vile-michango misikitini, makanisani, matamasha, harambee n.k

Alipoulizwa kuwa kuwa anapenda nini katika utumishi wake wa Ubunge, anasema anapendelea sana na atazidi kuhimiza/kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya aina  mbali mbali vya ujasiriamali, Sanaa n.k. kwa wa kina mama, vijana na wazee.

Kuhusu ajali aliyoipata

Anasema kwa sasa alirudi nyuma kidogo katika kufanya kazi hizo za kuikomboa jamii kiuchumi kutokana na ajali mbaya aliyoipata mwaka jana 2012 katika mteremko wa mlima Iwambi eneo la Mbalizi wilaya ya Mbeya ambayo ilisababisha kifo cha msaidizi wake.

‘’Ajali mbaya niliyopata mwaka jana ilinikwamisha mambo mengi nilikuwa nimepanga kuendelea kuteketeleza Ilani ya CCM lakini namshukuru Mungu afya yangu inaimarika na nitazidi kuwatumikia ndugu zangu wa Mbeya kutoka rohoni, ndivyo nilivyo asili mwana jamii hata kabla sijawa Mbunge, Mungu anisaidie niwatumikie kwa maendeleo na tukishirikiana wote vema tutajikomboa katika mengi’’ anasema Dr. Mary Mwanjelwa.

Kuhusu kugombea tena mwaka 2015, anasema kuwa Mungu akimpa kibali na afya njema atagombea na anaamini sifa anazo za kuendelea kuwa Mbunge wa Jimbo ama viti maalum.


HUYU NDIYE MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA, DR.MARY MWANJELWA


Hon. Dr. Mary M. Mwanjelwa is the Founder & Executive Chairman of Mbeya Women Trust Fund Foundation and current Member of Parliament, Special seat from Mbeya Region (Ruling Party-CCM).

She is a talented versatile generalist with extensive experiences and highly exposed internationally as well as in public community,communications/corporate relations, government relations, strategic management events managements, management and administrations without forgetting the community touch etc.

Has been giving out presentations as co-speakers in international forums i.e ACP/EU Women Forum (79 countries). Has been actively involved in this career profession cadre for more than 7 years before being a Parliamentarian.

She is the African Parliamentarians Network Against Corruption Tanzania Chapter President, she serves as an Executive Board Member for Africa of the same organization, she also serves as Deputy Secretary General of Women Parliamentarians in Tanzania,  she is also CCM Member of the National Executive Committee, and she is also Board Member of National Institute of Medical Research (NIMR) with Ministry of Health. She was in the Advisory Committee Member in the Hunting Blocks. Allocation in the Ministry of Natural Resources & Tourism as well as in the small Parliament committee of Operation Against Poaching in Tanzania.

Before being a Parliamentarian Dr. Mary Mwanjelwa was a Director for Population services international Tanzania and served as a Board Secretary as well from 2006-2010 – it's a Global Fund project under the Ministry of Health.

Prior to that she worked for Afrika Mashariki Gold Mine (Placer Dome-Canadian Mining Company) now known as Barrick Gold as a Liason Manager from 2001-2005.

She is currently persuing her Doctorate Degree at the Open University of Tanzania, “ Effect of Good Governance in Local Government”.  In 2010 she was awarded the Honorary Doctorate (PHD) in Humanity by California Seminary University (USA) United Graduate College & Seminary;  after engaging so much work of humanity/community.

She is also a Masters Degree Holder in Mass Communication from St. Augustine University – Tanzania.

She is a Post Graduate frorm the Centre For Foreign Relations-Kurasini, Dar es Salaam – Tanzania in International Relations with Diplomacy Management.

She is a mother of two boys.

IJUE BAADHI YA MITAA YA JIJI LA MBEYA

Hapa ni barabarakutoka eneo la Soweto kuelekea chuo kikuu cha TEKU na shule ya sekondari Southern Highland inayomilikiwa na , Philip Mulugo
Hili ni eneo la kungilia ofisi za SIDO Mbeya eneo la Block T. Jijini Mbeya.

Mbeya sasa inapendeza, hili ni eneo la kwenda Shule ya Msingi Samora, Airport Jijini Mbeya.


 Hapa ni barabara inayotok eneo la Esso, Jijini Mbeya kuelekea Forest Mpya, Jijini Mbeya. Sasa ni Lami tupu, hii yote inatokana na utekelezaji wa ilani ya CCM kwa msaada wa benki ya Dunia.


Saturday, June 21, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.06.2014.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,Ahmed Msangi.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA MWANAUME ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 35- 40 AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.974 CMC AINA YA CANTER LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA MAKAMBAKO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE BADO KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI KULIGONGA GARI T.777 AHF/T.107 BVB AINA YASCANIA LILILOKUWA LIMEHARIBIKA NA KUEGESHWA PEMBENI YA BARABARA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 19:15 JIONI KATIKA KIJIJI NA KATA YA IMEZU, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, DEREVA ALIKIMBIA  NA KULITELEKEZA GARI  MARA ENEO LA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI SWAYA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SIMON JULIUS (16) MKAZI WA IYELA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.745 NBA AINA YA CANTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA BARAKA ABDI (25) MKAZI WA IYELA KUPINDUKA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRAYA SAA 14:00 MCHANA KATIKA ENEO LA MAKABURINI IYELA, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WANNE WALIPATA MAJERAHA KATI YAO WANAWAKE WATATU NA MWANAUME MMOJA WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


KATIKA MISAKO:

MSAKO WA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKAKWA JINA LA ELIAS LUCAS (38) MKAZI WA KIJIJI CHA ITUMBI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 25.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 17:50 JIONI KATIKA KIJIJI CHA ITUMBI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.



MSAKO WA PILI:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BARAKA MWAMBUNGU (23) MKAZI WA KIJIJI CHA ITUMBI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI GRAM 500.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA ITUMBI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


MSAKO WA TATU:

MTU MMOJA MKAZI WA NAKONDE NCHINI ZAMBIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JAMES SILUMBWE (28) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NOTI BANDIA 02 ZA TSHS 10,000/= SAWA NA TSHS 20,000/= ZIKIWA NA NAMBA BU-7282385. 

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI KATIKA MTAA WA TUKUYU, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, MKOA WA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI NA MATAPELI PIA KUTOA TAARIFA ZA MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA NOTI BANDIA ILI WAKAMATWE.


MSAKO WA NNE:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA TIMOTH KAPALISYA (33) MKAZI WA KYELA  ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BIDHAA ZILIZOPOGWA MARUFUKU NA SERIKALI.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI KATIKA MTAA WA BENKI- MWANJELWA, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] AINA YA DOUBLE PUNCH ZIKIWA KWENYE MIFUKO MIKUBWA MITATU YA  SANDARUSI KILA MMOJA UKIWA NA UJAZO WA DEBE SITA [06] BAADA YA  KUINGIZWA NCHINI KUTOKA NCHINI MALAWI.

Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

DR. MWANJELWA ATAKA WAFANYABIASHARA MBEYA WAPATE NAFASI SOKO LA KIMATAIFA

WAKATI kukiwa na tetesi za kwamba baadhi ya wafanyakazi wa Jiji la Mbeya na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa Jijini hapa wamejigawia vyumba katika soko jipya la Mwanjelwa, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, ameiomba serikali kutupia macho soko hilo na kuhakikisha hata wafanyabiashara wa kawaida wanapata nafasi.

Hayo aliyasema jana wakati anachangia Hotuba ya Bajeti kuu ya serikali mjini Dodoma.

Alisema soko hilo kwa sasa licha ya kutokamilika kwa wakati, serikali kupitia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Jiji la Mbeya limepata mkopo mwingine wa Bilioni tatu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi na wamepata mkandarasi mpya.

‘’Kama unavyoelewa Mheshimiwa Spika, kule kwangu Mbeya, kuna soko la kimataifa na Waziri Mkuu anajua na katika miezi nane ijayo soko litakamilika na ninaomba Wizara ya Fedha itupatie gurantee ya 3.4 bilioni ili tuweze kupata mara moja na wafanyabiashara wote wanufaike na soko ambalo lina jina langu la Mwanjelwa’’ alisema Dr. Mwanjelwa.

Pia aliiomba serikali kuchepusha barabara ya magari makubwa kutoka Uyole mpaka Songwe Mbeya Vijijini, ambako kuna uwanja wa Ndege ili kusaidia kuondoa msongamano wa magari Jiji la Mbeya ambalo linapanuka kila siku.

Mbali na jambo hilo, alichangia mambo mbalimbali likiwemo suala la misamaha ya kodi inayotolewa na serikali kwa wafanyabiashara wakubwa, migodi na makapuni ya simu, huku akieleza kuwa serikali inapaswa pia kufufua viwanda ili kupunguza tatizo la ajira.

“Mheshimiwa spika, uchumi wa nchi tunaambiwa kuwa unakua sana, sasa watanzania hawana kipato na maisha yao yanazidi kushuka, sasa uchumi unakua kwa namna gani? Deni la taifa linatishia usalama wa taifa, ongezeko la asilimia 29 najiuliza je tutafika?’’ alihoji Mbunge huyo.

‘’Tumekuwa tunazungumzia kuhusu walimu, naishauri serikali walimu wasikatwe maana wafanyakazi wote Tanzania wanaokatwa, wakienda sokoni pia wanaendelea kukatwa tena, wakati wanakatwa kodi mishahara yao’’.

Alishangaa kuwa Bunge linaidhinisha bajeti lakini pesa haitoki na kwamba matumizi mengine yanatumika bila kuidhinishwa, hivyo alihoji kama bunge hilo linatUmika kama stempu au la.

Aliitaka Wizara ya fedha pamoja na wabunge kurudi bungeni kuelezana mrejesho wa matumizi ya fedha za serikali na kwamba ifike mahala wabunge wawe wakali na sheria kali zitungwe ili wanaochelewesha fedha au kuhusika kwenye Fund Location na fund department wawajibishwe, pesa zisipotolewa kwa wakati.

“Kuna kipindi nilisimama hapa na kusema halmashauri zote zilizo na hati chafu ziadhibiwe, kwanini mambo yanafichwafichwa, kuna nini? makampuni ya simu na madini mbona hatuambiwi mikataba yake na misamaha ya kodi? Watanzania wajulishwe na wawekwe wazi’’ alisema.

Alisema watanzania wa kawaida wanaumia kutokana na bajeti ya kutegemea pombe na sigala na vinywaji, kwasababu ndiyo wanaotumia vitu hivyo kila siku.

‘’Ninaomba sana, tuangalie jinsi gani tufufue viwanda vyetu kusaidia ajira kwa vijana wanaokimbilia mijini na haya ndiyo maendeleo yenyewe. Kwenye private sector kule watu wanafanya kazi hakuna rongorongo na hii PPP, itasaidia kufufua viwanda na kuongeza ajira’’ alisema.